LEAT WAKUTANA NA WABUNGE KUJADILI SERA NA SHERIA ZINAZOHUSU SEKTA YA UZIDUAJI

DODOMA

 

TIMU ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT), wamekutana na wabunge ambao ni wadau wa madini na  mazingira, kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha Sera na Sheria zinazohusu Sekta ya uziduaji, Mafuta, Gesi asilia na madini.


Mafunzo hayo yamefanyika Aprili 29,2023 Jijini Dodoma.


Akizungumza kwenye Mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) Dkt.Rugemeleza Nshala, amesema wamekutana na wabunge hao sababu wao ni watunga sheria, waone namna ya kuishauri Serikali ili Rasilimali za nchi zinufaishe watanzania na vizazi vijavyo.


Amesema baadhi ya vifungu katika sheria ya madini, vinapaswa kufanyiwa mabadiliko au maboresho ikiwamo na namna ya kuboresha mikataba ambayo nchi inaingia na makampuni ya uwekezaji kutoka nje ya nchi.


"LEAT tumekutana na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kujadili kwa pamoja Sera na Sheria zinazohusu Sekta ya uziduaji, sababu wao ni watunga sheria na wataishauri Serikali kupitia vikao vya Bunge na hatimaye nchi yetu itanufaika na Sekta hii ya uziduaji sababu ni Rasilimali ambazo zinakwisha,"amesema Dk. Nshala.


Nao baadhi ya wabunge ambao wanatoka kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini akiwamo Mbunge wa Msalala Iddi Kassimu, amesema mkutano huo umekuwa na manufaa sana, sababu wamejadili kwa pamoja na kuongeza uelewa namna ya kuisaidia Serikali, ili nchi ipate kunufaika na Rasilimali zake kwa kuboresha Sera, Sheria, na mikataba.


Aidha, katika mkutano huo ziliwasilishwa mada mbalimbali, ikiwamo Sheria katika Sekta ya uziduaji, mabadiliko ya Sheria na athari zake kwenye mapato ya madini, changamoto wanazokutananazo wachimbaji wadogo, pamoja na ulinzi wa Mazingira na haki za ardhi.

Dkt. Rugemeleza Nshala akiwasilisha mada kwa wabunge

Silas Olang akiwasikisha mada kwenye mafunzo hayo

Evans Rubara akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

Clay Mwaifwani akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo




0
0
0

Our   Partners