UCHAFUZI WA MAZINGIRA UMEKITHIRI NCHINI NA VYOMBO HUSIKA VIMESHINDWA KUPAMBANA NAO

Ndugu Waandishi wa Habari,

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kushangaza na kusitikisha sana ya uchafuzi na uharibifu wa mazingira unaofanywa nchini hasa katika Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Mara. Moja mnamo tarehe 5 hadi 6 Aprili 2022 kulikuwa na umwagikaji wa mafuta katika eneo la Forodhani (Ferry) na kutapakaa baharini na hivyo kuleta uharibifu mkubwa si wa mazingira tu bali pia viumbe wa baharini na vyanzo vya mapato kwa wavuvi na wale wanaotegemea sekta ya uvuvi. Mnamo tarehe 6 Aprili 2022 Mkuu wa Wilaya ya llala, Nd. Ng'wilabuzu Ludigija alitembelea eneo hilo na kuthibitisha pasi na shaka kuwepo kwa uchafuzi huo wa mazingira na kunukuliwa na vyombo vya habari https://www.youtube.com/watch?v=GIY31YTS 7Q akitoa tahadhari kwa wakazi wa Dar es Salaam kutonunua mafuta yaliyochotwa na watu ambao waliyachota na kuyatoa baharini. Hata hivyo alitoa tuhuma ya jumla kuwa mafuta hayo yalimwagwa baharini na meli isiyojulikana!

Kauli hiyo inashangaza na haingii akilini kwani eneo zima la Feri pale Kivukoni lipo chini ya Mamlaka ya Bandari ya Tanzania na ina mamlaka ya kudhibiti uchafuzi wowote ule wa mazingira ufanywao na meli. Kwamba "meli" hiyo hakuweza kubainika ni uthibitisho kuwa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania imeshindwa kutekeleza wajibu wake kama ambavyo imepewa na Sheria ya Bandari (Ports Act No 17 of 2004). leleweke kuwa hakuna meli yoyote 2 ile inayoweza kuingia katika maji ya ndani ya nchi yetu bila kibali cha nchi yetu na kuwa meli yoyote ile iingiayo katika maeneo ya maji ya nchi yetu inalazimishwa na sheria zetu na sheria za kimataifa kuheshimu sheria za nchi yetu. Na kwa kuwa meli zinazotia nanga katika bandari zetu zinakuwa na kibali basi ni kuwa "meli" hiyo ilipata kibali hicho na kama kweli ndiyo iliyomwaga mafuta hayo katika eneo hilo basi umwagaji huo uliruhusiwa au kufumbiwa macho na viongozi wa Mamlaka ya Bandari ya Tanzania. Aidha, uchafuzi huo pia umefumbiwa macho na Baraza la Taifa la Utunzaji Mazingira (National Environment Management Council (NEMC) ambalo lina mamlaka ya kuhakikisha kuwa uchafuzi wowote ule wa mazingira nchini unapingwa vita na wachafuzi wanachukuliwa hatua stahiki.

Soma tamko kamili na kupakua faili la PDF kwa kutembelea kiungo hiki

0
0
0

Our   Partners