MAFUNZO YA MFUMO WA UFUATILIAJI WA UWAJIBIKAJI KWA JAMII NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI WA KATA NA MABARAZA YA KATA BUTIAMA YAFUNGWA RASMI

KAIMU Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama mkoani Mara Revocatus Rutunda amehitimisha mafunzo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii na utawala bora kwa watendaji wa Kata Butiama na Mabaraza ya Kata.

Mafunzo hayo yalianza kutolewa Machi 27 mwaka huu na kuhitimishwa leo Machi 31, ambayo yalikuwa yakiendeshwa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo Lawyers Environment Action Team (LEAT).

Rutunda akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, ameipongeza Timu hiyo ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa kuwapatia mafunzo hayo viongozi wa ngazi ya Kata ambayo yamewaongeza maarifa katika utendaji wao pamoja na kwenda kudhibiti suala la uharibifu wa mazingira.

“Katika maeneo yetu kumekuwapo na uharibifu mkubwa wa mazingira, hivyo mafunzo ambayo mmepatiwa hapa yakawe chachu ya mabadiliko na kuzuia uharibifu wa Mazingira na kwenye mipango yenu ya Kata suala la Mazingira mlipe kipaumbele,”amesema Rutunda.

“Ili kutekeleza suala hili la kuzuia uharibifu wa Mazingira, naangiza kila Kijiji mkaunde Sheria ndogo na Afisa Mazingira simamie jambo hili na ndani yam waka huu sheria hizi ndogo ziwepo ambazo zitasaidia pia kuzuia uharibifu wa mazingira,”ameongeza Rutunda.

Naye Mwenyekiti wa Mafunzo hayo Magreth Kyanzi, akizungumza kwa niaba ya wwenzake, amesema mafunzo waliyoyapata yamewabadilisha kiutendaji na watakwenda kuwa viongozi wazuri, pamoja na kusimamia vyema Rasilimali za Maliasili na utunzaji wa mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama Revocatus Rutunda akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Mkufunzi wa mafunzo kutoka (LEAT) Hana Lupembe akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa mafunzo Magerth Kyanzi akitoa shukrani kwenye uhitimishaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye uhitimishaji wa mafunzo kutoka LEAT.
Washiriki wakiwa kwenye uhitimishaji wa mafunzo kutoka LEAT.
Washiriki wakiwa kwenye uhitimishaji wa mafunzo kutoka LEAT.
Washiriki wakiwa kwenye uhitimishaji wa mafunzo kutola LEAT.

Picha ya pamoja ikipigwa.
0
0
0

Our   Partners