Mkutano wa 27 wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP 27

Mwishoni mwa 2022 kumesheheni mikutano mbalimbali inayolenga kulinda mazingira. Sehemu ya mikutano hiyo ni mkutano unaofanyika kila mwaka kwa kukutanisha wadau mbalimbali juu ya mabadiliko ya Tabianchi, yaani Mkutano wa 27 wa Mabadiliko ya Tabianchi almaarufu kama COP 27.

Mkutano wa 27 unaofanyika Sharm el Sheikh, Misri unapokea kijiti toka mkatano kama huu uliofanyika jijini Glasgow. Mkutano wa 27 umekabidhi kijiti cha URAIS kwa Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri. Ndugu Shoukry atakuwa RAISI kwa mwaka mmoja kuelekea mkutano kama huu utakaofanyika mwaka 2023 katika Falme za Kiarabu.

Hivyo yote yanayojadiliwa na kuafikiwa chini ya mkutano wa 27 (yaani sasa) yatatajwa kama mafanikio na mikakati ya Sharm el Sheikh. Tukumbushe kuwa mkutano huu unajadili mabadiliko ya Tabianchi kwa ujumla wake.

Kuna mengi yanaendelea Sharm el Sheikh. Dhamira kuu ni moja nayo ni kujadili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kina. Wakuu wa nchi (na wawakilishi wao) hali kadhalika wamepata fursa mbalimbali za kufanya majadiliano. Kufika kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko nchini Misri ni mfano wa namna Sharm el Sheikh ilivyotoa fursa kwa wakuu wa nchi kushiriki kujadili, kuona na kufanya maamuzi juu ya masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Ikumbukwe kuwa mkutano huu ulioanza Novemba 8 na utakaoisha Novemba 18, 2022 umelata wadau mbalimbali. Sehemu ya wadau wa mazingira waliofika ni pamoja na nchi, serikali, makampuni, mataifa, Asasi za Kiraia (AZAKI), wafanyabiasha, wanawake, vyuo vikuu, vijana, kwa kutaja wadau wachache.

Wadau wote wanapata majukwaa mbalimbali kujadili masuala yanayowahusu wao na makundi yao. Kwa uchache, mambo ambayo yanajadiliwa ni pamoja na maji, misitu, nishati, wanawake, vijana, haki za binadamu, nishati mbadala, kilimo, plastiki nazo zimepata mijadala ya kutosha.

Nchi zinazoathirika zaidi nazo zinaendelea kudai uwajibikaji wa wachafuzi ili nchi zao zipate ahueni ya changamoto ya mabadiliko ya Tabinchi. Haya yote yanatokea jirani na matukio ya kimazingira ambayo yametokea nchi mbalimbali duniani. Ikumbukwe theluthi (1/3) ya Pakistani ilikua chini ya maji katika siku za karibuni. Je ni nini hasa kimejadiliwa huko nchini Misri. 

0
0
0

Our   Partners