UMUHIMU WA UTATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA YA USULUHISHI KATIKA KUKUZA UCHUMI ENDELEVU: WAJIBU WA MAHAKAMA NA WADAU

 

Ruaika Shauri, Mwanauchumi -LEAT


Binadamu hutofautiana mawazo na falsafa na sababu ya tofauti hizo, huja kuleta migogoro au mtafaruko kati ya pande mbili. Na tofauti hizo ambazo huleta migogoro inabidi itatuliwe. Na dawa ya mgogoro wowote ule inabidi uwe na utatuzi, na mojawapo ya kuwa na majibu ya utatizo ni kuwa na suluhisho baina ya wadaawa.

Suluhisho hilo hutolewa na mtu huru (mediator) ambaye hutokana na uzoefu wake wa kutoa suluhisho kwenye migogoro iliyopita. Njia hii ya usuluhishaji huweza kutumika badala ya kwenda mahakamani ambapo hatua zake za upatikanaji wa haki ni ndefu na kwa sababu pia hutumia mnyororo mrefu zaidi ya watu, hata gharama zake huwa kubwa zaidi.

Njia hii ya usuluhishi huongeza mahusiano na kuwa yenye nguvu zaidi, na mahusiano hayo huweza kuleta manufaa kiuchumi. Mahusiano hayo yaliyokuwa yameharibika , kwa kutumia usuluhishi unaweza kurejesha mahusiano hayo na wadau wengine mbalimbali kama mteja, mzabuni nakadhalika.

Njia hii ya usuluhishi pia haipotezi muda kama ambavyo ukitumia njia ya mahakamani. Njia ya mahakama ina hatua nyingi za kufuata inayofanya kuchukua muda mrefu zaidi ya njia ya usuluhishi.  Njia hii ni njia ya makubaliano tu kati makundi mawili au watu wawili ambao walikuwa wamepishana.

Njia hii ya usuluhishi pia sio lazima kutumia sheria na miongozo yake pia. Wadaawa hutumia njia kadha wa kadha za wao kufikia makubaliano. Huweza kuhusisha wadau mbalimbali kutatua kasoro kati ya pande hizo mbili.

Njia hii ya usuluhishi ni nzuri sababu pia haitumii gharama kama njia ya kwenda mahakamani ambako ni gharama sababu huhusisha watu wengi zaidi na wenye fani ya sheria, ambayo inabidi ulipie huduma ya wakili kukutetea mahakamani na huduma zingine za mahakama

Njia hii ya usuluhishi pia huweza kutumika sehemu ambapo hakuna huduma ya mahakama kutoa haki na usawa, hasa sehemu za vijijini ambako kuna maeneo wanakosa huduma hii.

0
0
0

Our   Partners