MRADI WA CEGO WACHANGIA ONGEZEKO LA MAPATO KIJIJI CHA ITAGUTWA

Monday, August 21, 2017|Number of views (1917)|Categories: CEGO-NRM
MRADI WA CEGO WACHANGIA ONGEZEKO LA MAPATO KIJIJI CHA ITAGUTWA


Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagutwa wilayani Iringa, mkoani Iringa Isaya Lubava amesema usimamizi wa maliasili katika kijiji chake umeimarika kwa kiasi kikubwa, hali inayochangiwa na ongozeko la uelewa kwa wananchi kuhusu wajibu wao katika usimamizi wa maliasili.Alisema hayo jana wakati wa mkutano wa marejeo na kuhitimisha mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unaotekelezwa na Timu Wanansheria watetezi wa mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa ufadhili wa shirika la Maenedeleo la kimataifa la Marekani (USAID) katika Wilaya za Iringa na Mufindi mkoani Iringa.

Lubava alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa utekeklezaji wa mradi huo, kijiji kimeweza kuongeza ukusanyaji mapato kutokana na kuunda kwa mpango wa usimamizi wa hifadhi ya kijiji.

“Tulibuni njia mbalimbali za usimamizi, yaani ulinzi wa hifadhi na mojawapo ni ufugaji nyuki, ” alisema.Mradi huyo ulianza kutekelezwa Novemba mwaka 2013 na utafika ukomo mwezi Novemba mwaka huu 2017.


Alisema kuwa kijiji chao kimechukuwa hatutua mbalimbali za kukabiliana na uharibufu wa misitu, hivyo wanajivunia mafanikio katika kukabiliana na matumizi yasiyo dumivu ya maliasili.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa LEAT imekuwa ikitekeleza mradi wa ‘Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili’ (CEGO-NRM).


Afisa Mradi Mwandamizi wa mradi wa CEGO-NRM, ndugu. Remmy Lema alisema mradi umetekelezwa katika vijiji 32 huku lengo kubwa likiwa ni kukuza ushiriki wa wananchi katika uhifadhi na usimamizi wa maliasili ili kupunguza umaskini na kuhakikisha kuwepo kuwepo kwa usimamizi dumivu  wa maliasili.


Alisema kuwa kuhitimishwa kwa mradi huo wa ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili ni chachu ya kuimarisha usimamizi wa maliasili katika mkoa wa iringa na nchini kwa ujumla.


Naye mwenyekiti wa bodi ya LEAT, Bw. Gosebert Kamugisha wakati wa kuhitimisha alisema kuwa LEAT itaendela kutoa wito kwa serikali kuendelea kuzisaidia taasisi za waruzuku wa mradi huo ili ziendelee kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa ajili ya kuyaendeleza malengo ya mradi.


Aidha, Bw. Kamugisha alisema kuwa LEAT inaendelea kutoa wito wa kusaidia na kuunga mkono Timu za Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii (UUJ) za wilaya na za vijiji zilizoundwa kupitia mradi huo ili ziweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.


Kamugisha alisema LEAT ilikasimisha baadhi ya shughuli kwa taasisi nne za waruzuku (sub-grantees) wake yaani; MBOMIPA, MJUMIKK, MUVIMA NA ASH-TECH wakati wakutekeleza mradi huo. Waruzuku hao walifundishwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa shughuli za mradi, uwezeshaji wa shirika na usimamizi wa fedha.


Please login or register to post comments.

«July 2018»
MonTueWedThuFriSatSun
2526272829301
2345678
9
2147

Israel’s attempt to demolish Palestinian village Khan al Ahmar contravenes international law

Israeli forces are forcibly displacing Palestinians as they attempt to demolish the Bedouin village of Khan al Ahmar in the occupied West Bank. Israeli forces are dragging away residents and protesters and attacking people as they resist being forcibly displaced from their homes. The Palestinian Red Crescent has reported 35 people wounded, with four taken to hospital. Our comrades at the Israeli rights group B’Tselem report nine people have been arrested.

Read more
1011

Prize Winners Network at the ELAW Annual Meeting in Tanzania

“Being amongst the Prize winners, one could feel a particular energy, the kind of energy that made me feel privileged to be part of the group.” — Makoma Lekalakala, 2018 Prize winner from South Africa

Read more
12131415
16171819202122
23242526272829
303112345