WANANCHI WA UHAMBILA ACHENI KUHARIBU VYANZO VYA MAJI NA MALIASILI ZENU

Mkutano wa Uhamasishaji jamii juu ya ushiriki wao katika usimamizi wa malisili katika kijiji cha Uhambila, wilayani Mufindi

Friday, May 19, 2017|Number of views (2100)|Categories: CEGO-NRM
WANANCHI WA UHAMBILA ACHENI KUHARIBU VYANZO VYA MAJI NA MALIASILI ZENU

Wananchi wa kijiji cha Uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho, Afisa Mradi wa mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili (CEGO-NRM) kutoka Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) upande wa wilaya ya Mufindi Bw. Jamali Juma, alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.

"Mkiangalia zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama zamani" alisema juma

Ukataji miti na uharibifu wa vyanzo vya maji unasababisha madhara mengi makubwa na ndio maana tunaona sasa kumekuwa na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababisha athari za moja kwa moja kwa mwanadamu na kwa Mazingira, Na ndio maana uharibifu huo husababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.

Juma alisema kuwa “dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu”.

"Ni kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu vyanzo vya maji. Kutokana na sheria ya misitu ya mwaka 2002 na Sheria ya maji namba 11 ya m waka 2009, zinatamka kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yoyote kuharibu maliasili hizo na zimetaja adhabu kwa yoyote atakayebainika kuharibu rasilimali hizo”, alisema Juma

Shirika lisilo la kiserikali la LEAT wametoa elimu ya Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili kwa miaka minne mfululizo kwa vijiji 32 vya mradi ambavyo vipo wilaya ya Iringa na wilaya ya Mufindi na kushirikiana kwa ukaribu na halmashauri za wilaya hizo kuendelea kuboresha Mazingira ambayo yapo chini yao.

Franklin Masika ambaye ni Afisa ughani wa shirika la LEAT kwa upande wa wilaya ya Mufindi, aliwataka wananchi kufuata sheria ya mazingira ya mwaka 2004 namba 20 na sheria ya maji namba 11 ya mwaka 2009 zinazoeleza wazi kuhusu kilimo cha vinyungu au kulima kandokando ya mto au kwenye vyanzo vya maji na kuna faini zimeorodheshwa. Hivyo sheria hizi sio ngeni, Isipokuwa zimeonekana kutotekelezwa, Ila ninawahasa kuanzia sasa mzingatie na kutekeleza sheria hizo kwani serikali imeanza kuzifuatilia kwa umakini zaidi.

"Mkiangalia kijiji cha uhambila kipo katika bonde la mto Ruaha hivyo wananchi mnatakiwa kuwa makini na hizi sheria kwa kuwa lengo la serikali ni kuboresha Mazingira ya kuutunza mto Ruaha Mkuu, ambao unahati hati ya kutoweka, na nyie ni walinzi namba moja wa mto huo "alisema Masika

Lakini Franklin Masika alizitaja baadhi ya adhabu zinazotokana na uharibifu wa Mazingira mfano kuchepusha maji, kukinga, kuchukua au kutumia maji kinyume cha sheria ni kosa la jinai na adhabu yake ni shilingi 300,000 na isiyozidi 500,000 au kifungo cha miezi miwili na kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na sheria hiyo.

Masika aliwataka wananchi wa kijiji cha Uhambila kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla ili kuboresha maeneo wanayoishi na kupunguza au kufuta kabisa milipuko ya magonjwa inayotokea mara kwa mara katika maeneo ya vijijini.

Chelsoni Kikoti, Amani Nyakunga na Reginandi Chalamila ni wananchi wa kijiji cha Uhambila waliiomba serikali zitafakari upya sheria hizo kwa kuwa zinawaumiza wananchi wa vijijini. Hii inatokana na mazoea ya kutumia maliasili zinazowazunguka kama chanzo cha kuwapatia kipato, Kwani wemekuwa wakitegemea sana kilimo cha mboga mboga kuendesha maisha yao.

"Hebu angalieni Mazingira haya tunayoishi hakuna njia nyingine ya kupata kipato zaidi ya kutegemea kulimo cha vinyungu, ambako tunalima mboga mboga tu. Jamani hee tuatakufa na njaa hebu muishauri serikali juu ya sheria hizo" walisema wananchi

Thomas Mtelega Afisa Mradi wa taasisi ya Mufindi Vijana kwa Maendeleo (MUVIMA) aliwaomba wananchi kulima kilimo cha kisasa kutokana na Mazingira wanayoishi na kuacha tabia za kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji mfano kulima mboga mboga ni rahisi unaweza kulima hata kwa kutumia maji machache na kwa kumwagilia.

"Kuna maji machafu ambayo tunayoyatumia majumbani kwetu, ni maji ambayo tunaweza kuyatumia katika Kilimo cha mboga mboga kwa kuchukua udongo na kuuweka kwenye gunia au visarufeti, ambavyo ukipanda mbegu unaweza kupata mboga nzuri na salama. Gunia au Sarufeti linaweza kuchuja uchafu wote na kuiacha mboga ikiwa salama. Ninawashauri wananchi kutumia njia hii ili kuondokana na ulimaji wa karibu na vyanzo vya maji. Hii itasaidia sana kuboresha Mazingira yanayowazunguka”, alisema Mtelega.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Uhambila Agnes Simba aliwashukuru shirika la LEAT kwa elimu waliyokuwa wanaitoa kwa miaka minne. “Elimu hii imetukomboa kwa kutambua umuhimu wa kushiriki katika kusimamia maliasili za kijiji. Mfano mpaka sasa tunatambua sheria ya Mazingira, Misitu, Maji na wanyama pori. Lakini pia LEAT imetuwezesha kutunga sheria ndogo ya kijiji ya usimamizi wa maliasili. Sheria ndogo hii itatusaidia kuhakikisha maliasili za kijiji zinatunzwa kwa matumizi ya kizazi hiki na kijacho.


Please login or register to post comments.

«February 2019»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728123
45678910