VIONGOZI WA KIJIJI CHA KIBADA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA NCHI NA KIJIJI KATIKA USIMAMIZI WA MALIASILI ZAO

Mkutano wa kijiji cha Kibada, wilayani Mufindi, wa Kuhamasisha wanakijiji juu ya ushiriki wao katika kusimamia maliasili

Thursday, May 18, 2017|Number of views (2045)|Categories: CEGO-NRM
VIONGOZI WA KIJIJI CHA KIBADA WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA NCHI NA KIJIJI KATIKA USIMAMIZI WA MALIASILI ZAO

Ili kuongoza au kusimamia jamii ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuondoa migogoro mbalimbali inajitokeza na itakayo kujitokeza kwa sababu ya kuzivunja sheria na taratibu hizo.


Hayo yamesemwa na Afisa Mradi wa Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa maliasili unaotekelezwa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) Bw. Jamali Juma wakati wa mkutano wa kijiji cha kibada kilichopo kata ya Saadani wilayani Mufindi Mkoani Iringa, kwa kuwataka viongozi na wananchi kutimiza wajibu na haki ili kukifanya kijiji kiwe na maendeleo.


Juma alisema kuwa “sheria na taratibu zilizopo hapa kijiji zitanatakiwa kufuatwa kwa ajili ya manufaa ya sasa na ya kizazi kijacho kwa kufanya hivyo itajenga amani na usimamizi dumivu wa maliasili za kijiji”.


"Leo hii usipofuata sheria na taratibu za kijiji hakika utakwazana na viongozi au wananchi na kupelekea migogoro ndani ya kijiji kwa kuwa sheria zinakuwa zimekiukwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977" alisema Juma


Aidha Juma aliwataka viongozi wa kijiji cha Kibada kuitisha mikutano ya kijiji na kuwasomea mapato na matumizi ili wananchi wajue wapi kijiji kimetoka kimaendeleo na ipi ni mipango na mikakati mipya ya maendeleo ya kijiji.


"Katika vijiji vingi unakuta migogoro mingi inayotokana na kutosomewa mapato na matumizi kwa sababu binafsi za viongozi husika hivyo ni lazima viongozi wa vijiji kuongoza vijiji kwa kufuata sheria na taratibu za kijiji" alisema Juma.


Lakini Juma aliwataka wananchi wa kijiji cha Kibada kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na Maliasili walizonazo na kuacha kuishi kwa mazoea ili kulinda mazingira na kurudisha hali nzuri ya Mazingira kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Alisema zipo njia mbadala zilizo rafiki kwa Mazingira, hasa kwa kulima kilimo cha kisasa kinachotumia teknolojia itakayomsaidia mkulima kujipatia mazao yake kwa upande mmoja na kutunza Mazingira yanayomzunguka kwa upande mwingine.


"Jamani kuna njia nyingi za kulima mboga mboga kwa njia ya kisasa ambayo haikulazimu kusogea ndani ya mita 60 kutoka kwenye kingo za chanzo cha maji, kwani hutahitaji maji mengi kwaajili ya umwagiliaji. Kwa mfano unaweza kuchukua Gunia au Sarufeti na kuuweka mchanga kisha kupanda mbegu za mboga na kumwagilia maji yaliyobaki baada ya kufanyia usafi wa nyumbani. Hii itasaidia kuvifanya vyanzo vya maji kuwa salama" alisema Juma.


Fadinard Yilikwipande, Shauri na Stephano waliitaka serikali kuangalia upya sheria ya kilimo. Kwani wao wanategemea kilimo cha mboga mboga kwaajili ya kujiongezea kipato. Kilimo hiki kinalimwa kwenye udongo mnyevumnyevu au karibu na vyanzo vya maji alimaarufu kwa jina la “Vinyungu”.


"Sisi tunalima kwenye vijaruba vidogo vidogo tu maarufu kama vinyungu wala hatuleti madhara yoyote ya uharibifu wa vyanzo vya maji na mbona miaka yote tulikuwa tunalima bila kuharibu Mazingira na serikali itambue kuwa Kilimo hiki ni cha kitamaduni sasa inatakiwa kutofautisha sheria za mambo ya asili au ya kiutamaduni"walisema wananchi wa Kibada.


Kwa upande wake Afisa habari wa LEAT Bi. Edina Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha Kibada kuzifuata sheria zilizowekwa za kulinda Mazingira na vyanzo vya maji hadi pale serikali itakapotoa tamko lingine kuhusu sheria hiyo.


"Jamani sheria ni msumeno hivyo mnapaswa kuzifuata kwa kuwa msipozifuta mtatiwa nguvuni na kupelekwa mahakamani hivyo itakuwa inawapunguzia nguvu kazi yenu na kupelekea usumbufu kwa familia zenu. Mimi nawaomba tiini sheria bila shuruti ili kuepukana na hayo matatizo" alisema Tibaijuka


Tibaijuka aliwashauri wananchi na viongozi wa kijiji cha Kibada kupeleka malalamiko yao kwa viongozi wa serikali, madiwani na wabunge wao ili kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto ya zuio la kilimo cha vinyungu lililotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu la kukataza Kilimo chochote kile kwenye vyanzo vya maji.


Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kibada, Bw. Philipo Nyavili aliwaomba viongozi wa serikali kuipitia upya sheria ya maji ya Mwaka 2009, kwa kuangalia utamaduni wa watu vijijini hasa kwenye suala la kilimo cha vinyungu kipindi cha kiangazi katika maeneo ya mabondeni, kwa kuwa wananchi wa Vijijini wanategemea sana kilimo hicho.


"Hivi kama huku wilaya ya Mufindi wakulima wanategemea Kilimo cha kulima kwenye mabonde maarufu kama Kilimo cha vinyungu kwa kupanda mboga mboga pamoja na mahindi kipindi cha msimu wa kiangazi"alisema Nyavili


Please login or register to post comments.

«February 2019»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728123
45678910